Wenye mizizi katika Baba
Wimbo wa kwenda juu.
Kutumaini kunaelezwa kijiografia. Wanaotumaini hawatikisiki kama Mlima Sayuni, na Baba yetu anawazunguka kama vile milima inavyoizunguka Yerusalemu. Utawala wa waovu hautabaki juu ya nchi hii, kwa sababu ungewashawishi watu wema kutenda maovu.
125 1Wale wanaomtumaini Baba yetu ni kama mlima Sayuni, usioweza kutikiswa bali udumuo milele. 2Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, ndivyo Baba yetu anavyowazunguka watu wake, tangu sasa na hata milele. 3Fimbo ya uovu haitakaa juu ya nchi waliyopewa wenye haki, ili wenye haki wasinyooshe mikono yao kutenda mabaya. 4Uwatendee mema, Baba yetu, wale walio wema, wale walionyoka mioyoni mwao. 5Bali wale wanaogeukia njia zao zilizopotoka, Baba yetu atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani iwe juu ya Israeli!