Ukuu wa Mordekai
10 1Mfalme Ahasuero akaweka kodi juu ya nchi na juu ya visiwa vya bahari. 2Je, matendo yake yote ya nguvu na uweza, na maelezo kamili ya ukuu ambao mfalme alimpandisha nao Mordekai, hayakuandikwa katika kitabu cha tarehe za wafalme wa Umedi na Uajemi? 3Mordekai Myahudi alikuwa wa pili baada ya Mfalme Ahasuero, mkuu miongoni mwa Wayahudi, aliyependwa na ndugu zake wengi, akitafuta mema ya watu wake, akinena amani kwa wazao wake wote.