Bildadi Anena Tena
25 1Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu: 2"Mamlaka na utisho ni vyake; hufanya amani katika mahali pake pa juu. 3Je, kuna awezaye kuhesabu majeshi yake? Je, nuru yake haichomozi juu ya kila mtu? 4Basi mwanadamu awezaje kuwa mwenye haki mbele za Mungu? Awezaje kuwa safi yeye aliyezaliwa na mwanamke? 5Tazama, hata mwezi hauna mng'ao, na nyota si safi machoni pake; 6sembuse mwanadamu, ambaye ni funza, na mwana wa Adamu, ambaye ni mdudu!"